Sunday, May 31, 2015

WASANII WACHANGA WAONYESHA UWEZO WAO NDANI YA MTAA KWA MTAA

Kama ilivyokawaida ya Nisha's film production huwa haiwaachi wasanii wachanga basi humo kwenye MTAA KWA MTAA wamefanya yao. Katika kitu ambacho hakikutegemewa ni wasanii hao wachanga kuonyesha uwezo wao wahali ya juu mpaka mtu ushindwe kutambua kama kweli hawa ndio mara yao ya kwanza au ni wakongwe katika sanaa. Kama huja nunua Dvd ya MTAA KWA MTAA kanunue sasa ili uweze kujionea uwezo wa wasanii hao wachanga katika sanaa ya uigizaji. Nisha's film production lengo lake kubwa ni kuwainua wasanii wa changa hivyo huwapa nafasi za kucheza katika movie zinazotoka Nisha's film zam kwa zam. Kama na wewe ni msanii mchanga na unahitaji kushiriki katika movie za Nisha's film basi fanya ku follow page zetu za instagram ambazo ni @nishabebee @nishasfilmproduction @ochu_255 na kwa wale waliopo facebook unaweza ku join katika group letu ambalo ni Team nisha films production au unaweza kulike page yetu Nisha's film production pia kama upo whatsapp unaweza kuwasiliana na Production manager wa Nisha's film bwana Othman kwa no 0789 586057.











Saturday, May 30, 2015

MASTAR WAIPOKEA MTAA KWA MTAA KWA KISHINDO


MTAA KWA MTAA ya pokelewa kwa kishindo na mastar katika movie zilizokubaliawa na mastar basi MTAA KWA MTAA ndio movie namba moja iliyo kubalika kwani kila mmoja aliisifia na wengine kuahidi kuitafuta maana kuanzia wasanii,ma producer,ma director pamoja na wanamziki na hata wale watu wenye majina makubwa hapa nchini oda kutoka nchi mbalimbali za zidi kumiminika. Kenya,Rwanda,Burundi,Congo pamoja na nchi za bara la ulaya wanapiga simu nakuulizia ni jinsi gani wanaweza kuipata movie ya MTAA KWA MTAA.
HONGERA SALMA JABU NISHA KWA MOVIE BORA YENYE KUELIMISHA NA KUBURUDISHA










Wednesday, May 27, 2015

NISHA ASHANGAZA MAMILION YA WATU



Msanii wa filamu mwenye jina kubwa na heshima kwa jamii Salma Jabu Nisha ashangaza watu wengi baada ya filamu yake ya MTAA KWA MTAA inayotoka kesho siku ya alhamis tarehe 28/05/2015 kuisha steps na mwakala nchi nzima kugombaniana,hivyo kuwapa kuwapa kazi tena steps intertainment kutoa nakala nyingi zaidi za filamu hiyo ya MTAA KWA MTAA ambayo  imeoneshwa kupendwa na kukubaliwa  sana na mashabiki  kabla haijatoka, imeitwa maajabu kutokana kwamba filamu za star huyo asiyekuwa na scandals,mwenye sifa uchapakazi ‘’NISHA’’ kuvunja  record kazi zake kwa mauzo na kumfanya azidi kung’ara na kutoa filamu kali kupita zote kila atoapo,filamu hiyo kali ya MTAA KWA MTAA amewashirikisha  waigizaji mahiri kama Asha book,Hemedy Suleiman,Tausi Mdegela,Diana Kimary huku motto wake Nisha Iptysam Othman akionesha kung’ara zaidi naye,MTAA KWA MTAA imekuwa kiburudisho kikubwa haswa kwa kuonekana Nisha na Asha Boko kwenye mavazi ya Kitrafic huku kila mtu akitamani kujua ndani kuna nini na imekuwaje wakali hawa kuwa katika mavazi hayo. MTAA KWA MTAA itatoka kesho tarehe 28/05/2015 Mungu ibariki Mtaa kwa Mtaa ,ibariki Nisha’s film production,wabariki wasanii wanaojituma Tanzania.

Hongera Nisha MTAA KWA MTAA itazidi kufanya maajabu na kushangaza zaidi.





Sunday, May 24, 2015

ANGALIZO KWA WAANDAAJI WA TUZO

Kwanza napenda kuwapongeza wasanii wote ambao wanafanyiwa hujuma ili washuke kisanaa lakini matokeo yake wanapambana nakuendelea kusonga mbele ninachopenda kuwaambia TUZO siyo kitu kinachokufanya uwejuu bali juhudi zako katika kazi heshima na upendo kwa kila mtu ndio TUZO muhimu katika kazi yako ya yasanaa kwani itakuongezea mashabiki na kukupa maendeleo. Baada ya kuandika hayo narudi sasa kwenye mada kuu. Kwanza kabisa napenda kuanza kwenye TUZO zilinzo anza muda kidogo ambazo ni TUZO za KILIMANJARO MUSIC AWARDAS hizi TUZO zilianza kwa kasi sana watu wengi walikuwa wakizifuatilia na kuwapigia kura wasanii wanaowapenda lakini walikuja kuboronga pale walipoenda kinyume na wapigaji kura hadi leo hii tunaona TUZO za KILIMANJARO MUSIC AWARDS zipo lakini zimepoteza mvuto kama zamani na hata wapigaji kura wamepungua sio kama zilivyoanza.  Naomba tuhamie upande wapili kwenye hizi TUZO zilizoanza ambazo nazenyewe zimeshaanza kufanya ndivyo sivyo. TUZO ZA WATU hili jina ni tata kidogo kwa maana linamaana mbili maana ya kwanza Tuzo za watu yaani kuna watu maalum wameekewa hizo TUZO ndio maana ukaambiwa TUZO ZA WATU maana ya pili ambayo ndio waisema wao nikwamba watu wanawapigia kura wasanii wanao wapenda ili wagombanie hizo tuzo ndio maana ikaitwa TUZO ZA WATU hapa staki kuongea mengi kwa maana wenyewe mejionea katika wanaogombania 99% waliokuwepo ukumbini ndio walochukua TUZO. Hayo yote tisa kumi ni kwenye TUZO zililizo tolewa jana tuzo za TANZANIA FILM AWARDS ni TUZO mliboronga kupindukia kwanza mlichemka kwenye kupangalia kugombania hizo tuzo halafu jambo jengine kubwa mlilonishangaza TUZO mmeandaa wenyewe halafu nanyie wenyewe mpokatika kugombania kisha nyienyie ndio mnashinda jamani hamjui hatakula nakipofu. MWAKIFWAMBA hapa hamjengi bali mnabomoa kwani wasanii wenyewe wataanzakuchukiana pili mtajenga matabaka ya mashabiki na hapo ndio uhasama utazidi kwa wasanii. Napia mtasababisha wasanii wasiwe wana shiriki kwenye TUZO. lamwisho ninalopenda kuwaambia waandaaji wa hizi tuzo MSANII HAPANDISHWI KWA KUPEWA TUZO BALI MSANII ANAPANDA JUU KWA KAZI NZURI NA BORA.



Friday, May 22, 2015

NISHA'S FILM SOKONI TENA

Kampuni ya Nisha's Film Production yatarajia kuingiza sokoni movie yao mpya inayo julikana kama MTAA KWA MTAA akiongea hayo Bwana Othman Thiney ambaye ni Production Manager wa Nisha's Film Bwana Othman amesema MTAA KWA MTAA ni Movie nzuri ambayo Story yake haijawahi kuchezwa hapa Bongo anacho waomba watu wanunue cd original ili kuendeleza sanaa ya hapa nyumbani. MTAA KWA MTAA INATOKA MWISHO WA MWEZI HUU