Friday, January 29, 2016

KIBOKO KABISA YA PASUA ANGA AFRIKA MASHARIKI

KIBOKOKABISA ni Filamu ya kitanzania iliyotengenezwa nchini Tanzania ambayo inaweza kutazamwa duniani kote na rika lolote. Ni filamu yenye kuelimisha na kuburudisha pia ni filamu ambayo imechukua muda mrefu kutokana na kuandaliwa mazingira ya kurekodi vipande vya filamu hiyo. Nisha`s Film Production ni kampuni ya kwanza Tanzania inayo wathamini wasanii wachanga kwa kuweza kuwapa nafasi katika filamu zake ili kuweza kuonyesha uwezo wao. Ndani ya KIBOKOKABISA wasanii hao wamecheza nafasi kubwa nakwa uwezo mkubwa mpaka inakuwa ngumu kugundua kama wasanii hao ndio mara yao yakwanza kwenye game. KIBOKO KABISA IMEINGIA SOKONI IJUMAA YA TAREHE 29 MWEZI WAKWANZA MWAKA 2016
MARIAM BHAO

JENIFER TEMU

FRIDAUS KHATIBU

HEMEDY CHANDE

TUNU KHAMIS

Saturday, January 23, 2016

NISHA AMILIKI BAND YAKE

Mwana dada Salma Jabu Nisha aanzisha bend yake aliyoipa jina la movie yake mpya inayoitwa ``KIBOKOKABISA`` Bongohood ilipo fanya mahojiano naye nakumuuliza kwanini kaamua kuiita jina la movie KIBOKOKABISA  ndipo alipofunguka haya ``Nimeamua kuiita KIBOKOKABISA kutokana na Band yenyewe kwanza wapigaji vyombo vya Band hiyo, Vyombo  vya Band hiyo yani ukibahatika kuiyona live ndio utaamini kama ni KIBOKOKABISA pia napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa napenda kuwapa burudani basi mwisho wa mwezi huu NISHA`S FILM PRODUCTION itaachia movie yetu ya KIBOKOKABISA napia tutaachia video na audio ya Mziki kutoka KIBOKOKABISA BAND``
SALMA JABU NISHA KATIKA POZI
NISHA A.K.A KIBOKOKABISA










                                                                                               IG@nishabebee
                                                                                               IG@othman26square

Tuesday, January 12, 2016

NISHA`S FILM PRODUCTION YAWAFUTA MACHOZI WASANII WACHANGA

Ile kampuni kubwa Nchini Tanzania ya mwana dada mashuhuri mwenye roho ya kizungu Salma Jabu Nisha ya wafuta machozi nakuwafungulia njia wasanii hao kwa kuwapa nafasi walizokuwa wakiziota kila siku za kucheza movie katika nafasi kubwa ambazo huchezwa na wasanii wenye majina makubwa. Wasanii hao wachanga wafunguka nakumshukuru sana kwani Mastar wenye moyo kama wake niwachache hivyo wamuomba asivunjike moyo aendelee na moyo huo huo wamuahidi kufanya vizuri zaidi ya walivyofanya kwenye movie yao mpya waliyoipa jina la ``KIBOKOKABISA``
KIBIKOKABISA ni movie mpya yenye kuelimisha,kuchekesha pia kuburudisha iliyofanywa na kampuni ya Nisha`s Film Production filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwisho wa mwezi huu



KWA TAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUTEMBELEA ACCOUNT ZA INSTAGRAM
@nishabebee @othman26square @teamnisha @nishasfilmproduction

Friday, December 4, 2015

NISHA`S FILM PRODUCTION WAJA KIVINGINE

Ile kampuni inayoongoza kufanya vizuri upande wa filamu yaja kiaina yake. Nisha`s Film Production imeamuakuchukua kundi kubwa la wasanii wachanga na kuwapa nafasi kubwa kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao na pamoja kutimiza lengo la kampuni hiyo ya kuwanyanyua wasanii hao wenye ndoto za kuwa mastar wakubwa ndani na nje ya nchi yao ya Tanzania. Wasanii hao nao hawakulaza damu waliweza kuonyesha uwezo wao mpaka kuwa sawa na wale mastar hivyo kuwa vigumu kuwatambua kama ndio kwanza wanaanza Game hiyo.       MZIGO MPYA SOON UTAINGIA MTAANI


Kwa taarifa zaidi mfollow Production Manager wa Nisha`s film @ochu_255

Wednesday, July 15, 2015

NISHA AMEJIOA MWENYEWE , WABONGO WASHIKWA NA BUTWAA

Usipo staajabu ya Mussa utayaona ya Farao...  huo ni msemo ambao umejitokeza katika vinywa vya watu huku wakibaki mdomo wazi baada ya kushuhudia Mwanadada NISHA (SALMA JABU) Akitoa kali ya mwaka...
Msanii wa Comedy ambae anakadiriwa kua ni wapekee wa kike Africa Mashariki ikiwemo Kenya Uganda na Tanzania katika nyanja a uchekeshaji..... Akiwa nchini China nchi iliyogubikwa na Teknolojia ya hali ya juu... NISHA alitangaza kua ameamua kujioa yeye mwenyewe... huku Aina hiyo ya ndoa ikiwa na Sitntojua kua ni ya kabila gani na kwanini aliamua kuichagua China kua ndio sehemu pekee ya kutekeleza jambo hilo....huku akivaa mavazi nusu nusu... aina hii inatambulika kama (Shemale) duniani.. huenda akawa msanii na mtu wa kwanza kufanya tukio hili la pekee nchini...
Tukirudi katika maadili ya nchi Tunagundua kua aina hii si moja kati ya zile ambazo zimekatazwa kwani ameamua kujimiliki mwenyewe..bila kuvunja sheria...za maadili ya nchi.
Hivyo sheria ya nchi haiwezi kumtuhumu kama wanavyotuhumiwa wasanii wanapovunja maadili ya nchi huko ughaibuni.
AWA GUMZO CHINA
Msanii NISHA amekua akiwaacha wananchi wa jamii ya CHINA meno nje hasa anapokwenda katika moja ya hotel nchini humo kwa lengo la kujipatia milo ya mchana.asubuhi ama usiku.. kwani amekua akiagiza vyakula vya aina ya nchi hiyo na hujitahidi kula kama amezaliwa huko.
Muonekano na kuongea kwake kuliwachekesha sana Wachina katika mitaa ya Nchini humo hasa alipokua katika mizunguko... huku akizidi kuchana shavu baada ya kupokea mialiko katika sehemu mbali mbali muhimu...ikiwa hasa ni kuiongelea sanaa ya Tanzania...na ubora wake..
AJIFUNZA
Fursa ya mwanadada NISHA kutembelea katika uwanda wa nchi hizo... Alionekana kujifunza mengi sana hasa swala la sanaa na Mazoezi.. kitu ambacho wasanii wa China wamekua wakiweka kipa umbele sana.. tofauti na Tanzania.. wasanii wanaona sanaa na mazoezi ya mwili ni vitu viwili tofauti.
Blog hii ilijaribu.. kumtafuta mwanadada NISHA kwa mazungumzo ila bila mafanikio.. kwani amekua akizongwa na shuhuli zilizompeleka huko za kisanaa....
AWA TISHIO
Safari ya NISHA na uwepo wa huko China kuna weza kua Tishio kwa wasanii wa Bongo kwani huenda akaendelea kuliteka soko la filum  Bongo kwa kile kinachodaiwa huenda  akaanguka mikataba na ma kampuni makubwa ya utoaji Filum za huko China.
KILA LA HERI SALMA JABU NISHA...




Wednesday, June 24, 2015

KOMEDI KUMPELEKA NISHA UGHAIBUNI

Sikutaka kusema mapema ila wameniwahi,..
😢tukijaaliwa na ahsante M'Mungu we ni mwema sana... Kikubwa ahsanteni sana mashabiki zangu wote,nyi ndo mnaotenda haya.
Management yng yote ahsante...
#MTAAKWAMTAA ahsante 😢😭dah
Nisha punguza comedy haikufai.. guyz kwny ugali usichague kikubwa kiwe halali ☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆

Monday, June 1, 2015

WABUNGE NA MAWAZIRI WAISIFIA MTAA KWA MTAA

Baada ya kuona Mastar wakiisifia MTAA KWA MTAA sasa Nisha apata msg kutoka kwa wabunge pamoja na mawaziri wakimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya MTAA KWA MTAA. Ndani ya hiyo movie kuna mastar nao waliofanya yao kati ya mastar hao ni Asha Boko,Hemed Suleiman,Diana Kimary,Tausi Mdegela pamoja na mtoto wake Salma Jabu Nisha ambaye ameonyesha uwezo mkubwa anajulikana kama Iptysam Othman. Kama ilivyo kawaida ya Nisha's film huwa haiwachi wasanii wachanga nao wakafanya yao humo.